Sunday, September 4, 2016

NILITAKA KUONDOKA PSG''MATIUDI''



Kiungo wa Paris Saint-German Blaise Matiudi amethibitisha juu ya iliyokuwa nia yake ya kutaka kuondoka kwa mabigwa hao wa ligi kuu ya ufaransa Ligue 1 kipindi cha usajili uliomalizika wiki iliyopita. Kiungo huyo alihusishwa na mipango ya kujinga na Juventus ya Italia, Matiudi alichukizwa na mabingwa hao wa Ligue 1 kukataa kumruhusu kutimkia Italia kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Mino Raiola.


''Mchezaji mwenyewe alithibitisha kuwa uhamisho umefungwa''.


''Ndio nilitaka kuhama lakini klabu iliamua mimi kubaki na ingekuwa vinginevyo basi ningekubali hilo'',aliiambia Telefoot.''Ni kweli kwamba nilikuwa kwenye kipidi kigumu kwangu ambacho nilikuwa na ndoto na ndoto haikutimia''.

''Hata hivyo, sio kwamba siko na furaha PSG , mbali na hayo, kwa kweli nina furaha kuwa hapa''.

''Kuna kocha mpya na ninajua kwamba ana imani kubwa na mimi, tumejadili hili nadhani kila kitu kitakuwa sawa''.

Juventus walimtaka Matiudi kuziba pengo lililoachwa na mfaransa mwenzake Paul  Pogba alierejea Manchester United kwa rekodi kubwa ya usajili ya euro 105 million.

Hata hivyo kocha mpya wa PSG Unai Emery matarajio yake ni kumuona mchezaji huyo kwenye kikosi chake.



 
 

No comments:

Post a Comment