Sunday, September 4, 2016

OZIL AMEITAKA NO.10 ARSENAL



Mesutz Ozil ameitaka jezi namba 10 ya Arsenal iliyokuwa ikivaliwa na Jack Wilshere aliejiunga na Bournemouth. Ozil amezungumzia nia yake ya kuvaa jezi namba 10, kutokana na kukosekana kwa Jack Wilshere, huku kukiwa na mazungumzo na Arsenal juu ya mkataba mpya.

Ozil ambae ameanza kuvaa jezi namba 10 kwenye timu ya Ujerumani baada ya Lukas Podoski aliekuwa anavaa jezi hiyo kustaafu kuichezea timu hiyo na kusema kuwa angependa kuvaa namba hiyo akiwa Arsenal, baada ya Wilshere kujiunga kwa mkopo na Bournemouth na kusema kuwa sasa ni wakati wake kuvaa namba anayoipenda akiwa Emirates Stadium.
   
''Iko huru sasa na nia uhakika wa kuipata'' Ozil aliliambia gazeti la Ujerumani la Express.

''Nilikuwa navaa hii namba nikiwa na Ujerumani miaka iliyopita lakini Lukas Podolski  aliitaka pia na alikuwa na nafasi nyingi za kucheza zaidi yangu''.

''Hakika hii namba ni haki yangu kama mchezaji'' aliongeza''.

''Kwangu hii namba ina maana kubwa kwangu. Ni namba niipendayo na mashujaa wa mpira wa miguu kama Zinedine Zidane, Pelle na Diego Maradona walivaa namba hii''.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani anaamini mazungumzo kati yake na klabu yake ya Arsenal yatakuwa mafupi.

''Wakati huu nataka kuzingatia majukumu yangu kwa timu ya taifa'' Ozil alisema. Kwasasa tunaangalia kuendelea na mazungumzo. 

Ozil's mechi yake inayofata kwa Arsenal itakuwa nyumbani dhidi ya Southampton, baada ya kumalizika mechi za kitaifa.









No comments:

Post a Comment