Wednesday, September 14, 2016

AZAM NA SIMBA SEPTEMBA 17 TENA, AZAM YAKABIDHIWA NGAO YAO



Hapo jana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilibadili tena ratiba ya pambano kati ya Azam FC na Simba SC. Na kueleza kuwa litafanyika kama ratiba ya hapo awali ilivyopangwa Septemba 17 na sio tena Septemba 21. 


Mechi hiyo ilipelekwa mbele kufuatia kuipa nafasi timu ya taifa ya  vijana U17 ya Congo Brazzavile kufanya mazoezi dhidi ya mchezo wake na Serengeti Boys Septemba 18 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  

Huku Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba kwa mujibu wa kanuni ya 6 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kipengele cha 5 na 6, ameridhia mchezo huo kufanyika Uwanja wa Uhuru hapo Septemba 17, 2016 na kufuta upotoshwaji unaofanyika kwenye mitandao ya kijamii.  

Kawemba alizungumza hayo mara baada ya kupokea Ngao ya Hisani halisi mara baada ya tuzo hiyo kufika jijini Dar es Salaam ikitokea China pamoja na vifaa vingine . Itakumbukwa kwamba awali Agosti 17,2016 mara baada ya kuifunga Young Africans kwa mikwaju ya penati, Azam walipewa Ngao ya mfano.      

Huku chanzo kingine kikisema kuwa Azam wataisubili Simba kwenye Uwanja wao wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na sio Uwanja wa Uhuru sababu wao watakuwa wenyeji wa mchezo huo na hivyo watacheza kwenye uwanja wao na sio kwingine.     

 

No comments:

Post a Comment