Wednesday, September 14, 2016

MESSI APIGA HAT-TRICK BARCA IKIUA 7-0 NOU CAMP







Akiendelea kuthibitisha ubora wake kwa wanaompinga Lionel Messi hapo jana alifunga magoli 3 kati ya 7 kwa timu yake ikiisambaratisha vibaya Celtic kwenye mchezo wa kwanza kwenye kundi C. Wakiwa nyumbani Barcelona waliweza kujipatia magoli hayo kupitia wachezaji wake Lionel Messi dakika ya 3,27 na 60,Neymar 50,Iniesta 59, na Luis Suarez akitupia magoli 2 dakika ya 77 na 88.   

PSG wakitoka sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Parc des Princes, huku goli la PSG likifungwa na Cavani dakika ya 1 na Suarez akisawazisha ndani ya dakika 78.      


Huku mechi kati ya Manchester City na  Borrusia Monchengladbach ikiahirishwa kutokana mvua kubwa kunyesha na kujaza maji katika uwanja wa Etihad Stadium, na mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo hii siku ya Jumatano.       


Michezo mingine iliyoendelea hapo jana ni Atletico Madrid 1-0 PSV, Bayern Munich 5-0 Rostov ,Benfica 1-1 Beslkitas ,Basel 1-1 Ludogorem, D.Kylv 1-2 Napoli.     


Na leo kutakuwa na michezo ifuatayo

Leverkusen vs CSKA Moscow
Tottenham   vs Monaco
R.Madrid     vs Sporting CP
Legia            vs B.Dortmund
Club Brugge vs Leicester City
Porto            vs Kobenhavn
Lyon              vs Dinamo Zagreb
Juventus       vs Sevilla.

No comments:

Post a Comment