Monday, September 12, 2016

BALE NI MCHEZAJI BORA DUNIANI- REDKNAPP


Akiendelea kujenga nguvu kwenye klabu na timu yake ya taifa, Gareth Bale amepewa sifa na kocha wake wa zamani Harry Redknapp.   


Kocha huyo aliekuwa akiona maendeleo ya Bale kwa kipindi cha misimu nne akiwa Tottenham Hotspurs anashawishika kwamba mchezaji huyo amekuwa bora toka ajiunge na Real Madrid.   


''Bale ana kila kitu, ana nguvu ,yuko imara, ana pumzi na anaekimbia umbali mrefu na mashuti mazuri'', alisema Redknapp.   


''Kipindi anajiunga Madrid, nilisema atakuwa nyuma ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, lakini sasa anachofanya ni kupigania nafasi yake ya kuwa juu.''   
 
Na alipoulizwa juu ya mchezaji huyo kama anaweza kushinda Ballon d'Or, Redknapp alisema, ''Nadhani angeweza kushinda mwaka huu kama atakuwa mzuri kwenye Ligi ya Mabigwa.    
  

Huu ni msimu wa nne kwa Bale toka awe mchezaji wa Los Blancos na kila mechi anapiga hatua mbele kuwa mchezaji bora zaidi.    
 
 Kuwepo kwake kwenye uteuzi wa Best Player in Europe imempa nguvu na kujiamini ya kuwasogelea wachezaji bora wawili wa kizazi hiki cha sasa (Messi na Ronaldo).    


No comments:

Post a Comment