Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amepanga kumuanzisha mchezaji wake kinda Marcus Rashford kwenye mechi yao dhidi ya Feyenoord alhamisi ijayo.
United waliopoteza 2-1 dhidi ya City jumamosi iliyopita wameelekeza nguvu zao kwenye mechi dhidi ya Feyenoord kwenye Europa League ambapo United watasafiri Uholanzi kwa ajili ya mechi hiyo. Na baada ya hapo watacheza na Watford kwenye Premier League September 18,2016.
Kinda huyo ana magoli 8 katika mechi 18 alizoonekana na United katika michuano yote klabuni hapo.
Rashford ambaye bado hajaanza kikosi cha kwanza chini ya Mourinho lakini Mreno huyo yuko tayari kubadilika juu ya hilo kwenye Europa League.
''Kwangu mechi inayofata ni kubwa dhidi ya Feyenoord na mechi hiyo ataenda kucheza. Hilo ndilo jambo ninaloweza kusema,'' alisema Mourinho.
''Nimeshamuamini kabisa, najua kuwa mustakabali wake wa baadae juu ya kipaji chake atakuwa ni mchezaji mzuri.''
Rashford alieingia kipindi cha pili baada ya Mourinho kubadili mfumo wa 4-3-3 uliomuwezesha kinda huyo kucheza kushoto, ni kwenye mechi waliyoifunga Hull City alicheza kama stireka pamoja na Ibrahimovic.
Kocha huyo alisema ''pia kuwa kinda huyo ni namba 9, lakini kama utataka acheze sehemu tofauti na hiyo tunahitaji kumboresha, lakini nafasi yake ndio hiyo. Kawaida watu wanaangalia kipaji kwenye soka lakini nafasi ni muhimu sana na yeye ameonyesha hilo mara moja. Rashford anaweza kucheza peke yake au tukawachezesha pamoja na Ibrahimovic kama ambavyo tulivyofanya dhidi ya Hull City.''
Mechi iliyopita dhidi ya City kocha huyo alisema kuwa aliona City ni wadhaifu kwa upande wao na kinda huyo alipoingia kipindi cha pili,aliweza kuwapa kile ambacho walishindwa kukipata kutoka kwa Mkhitaryan na Lingard ndani ya kipindi cha kwanza.
Na alipoulizwa juu ya wachezaji hao kuogopa nafasi zao kikosini alijibu kuwa kiwango pekee ndio anachotazama na ukiniuliza kuwa wataenda kucheza dhidi ya Feneyoord jibu ni hapana, na sio kama ni adhabu bali ni maamuzi tu ya nafasi tuliyopo kwahiyo naenda kuchezesha wachezaji wengine.


No comments:
Post a Comment