Saturday, September 24, 2016
BARCELONA BILA MESSI YAIPIGA SPORTING GIJON 5-0
Barcelona leo imeweza kushuka dimbani bila nyota wao Lionel Messi na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Sporting Gijon kwenye uwanja wa El Molinon.
Luis Suarez na Rafinha kila mmjoa akifunga bao ndani ya kipindi cha kwanza na mpaka wanaenda mapumziko walikuwa wakiongoza kwa mabao mawili bila, na kipindi cha pili mabao ya Neymar ya dakika 80 na 88 na Arda Turan dakika ya 85 yakaifanya miamba hiyo ya LaLiga waondoke na pointi tatu muhimi dhidi ya weneyeji wao hao uwanjani hapo.
Katika mchezo huo ambao matumaini ya kurudi mchezoni kwa Sporting Gijon yalipotea baada ya Alberto Lora kutolewa nj'e kwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea madhambi Sergi Roberto.
Kama vile katika kujihami kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Jumatano ijayo dhidi ya Borrusia Monchengladbach alimpuzisha Sergio Busquets ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Denis Suarez huku nafasi ya Luis Suarez ikichukuliwa na Paco Alcacer.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment