![]() |
| Mchezaji wa Las Palmas Araujo akishangilia bao lake la dakika ya 85 |
Vijana wa Zinedine Zidane walijihakikishia kuondoka na pointi tatu ugenini hapo baada ya Marco Asensio na Karim Benzema kufunga mabao ambayo yaliwafanya kujihakikishia ushindi huo. Lakini mchezaji wa Las Palma, Tana alisawazisha ndani ya dakika ya 38 baada ya Asencio kuifungia Madrid bao la kuongoza dakika ya 33 na mpaka timu hizo zinaenda mapumziko matokeo yalikuwa 1-1. Na ndani ya kipindi cha pili Karim Benzema aliisawazishia Madrid dakika ya 67, lakini Araujo ndani ya dakika ya 85 akazima matumaini ya Madrid kuondoka na pointi tatu toka kwao.
![]() | |
| Bale akiwa aamini kilichotokea baada ya mpira kuisha . |
Lakini kwa matokeo hayo Madrid bado wako kileleni, Bale alisema kuwa hawako sawa kwa kuondoka bila ya kupata pointi tatu.
''Tumehudhika kwa kutoshinda.'' alisema.
''Bado tunabaki kuwa hatujafungwa katika Ligi, lakini jambo la muhimu ni kushinda pointi tatu.''
Bale aliongezea na kusema kuwa ''hatukuwa na bahati na nafasi tulizopata, lakini tunatarajia kucheza na Dortmund na itatubidi tufanye kweli.
''Hatukuwa na bahati, lakini mpira ndiyo ulivyo.''
Madrid watasafiri mpaka Ujerumani kwa ajili ya mchezo wa Klabu ya Mabingwa dhidi ya Borrusia Dortmund Jumanne ijayo.


No comments:
Post a Comment