Friday, September 23, 2016

BARCELONA NI KLABU PEKEE KWA LIONEL MESSI- FABREGAS



Baada ya kocha wa timu ya Taifa ya Argentina Edgardo Bauza kulalamika kuwa klabu ya Barcelona haimjali mshambuliaji wao alieumia Lionel Messi, baada ya Barcelona kuwaambia Argentina kuwa wamuangalie mchezaji huyo, ambaye atakaa nj'e kwa wiki tatu kuuguza majeruhi yake huku akikosa michezo mitatu ya klabu yake na miwili kwa taifa lake.
Lakini kiungo wa klabu ya Chelsea Cesc Fabregas amepinga kauli ya kocha huyo na kusema kwamba Barcelona ndio klabu pekee inayoweza kumuangalia nyota huyo wa Argentina. 

Fabregas na Messi walicheza pamoja kwa misismu mitatu, kipindi Mhispania huyo akiwa na miamba hiyo ya LaLiga kuanzia 2011-2014.  

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, amesema kuwa hana shaka na Barca kuwa ndio wenye uwezo wa kumuangalia Messi, ambaye sasa anauguza majeraha ya misuli. 

''Messi ni bora duniani bila shaka yoyote,'' Fabregas aliiambia Cadena COPE.  

''Nadhani ni klabu pekee duniani inayoweza kumpa huduma zote na kumuangalia Messi. Wameshafanya hivyo katika miaka ya hivi karibuni. Siku zote wamekuwa wakimuangalia kwa umakini. Ni klabu bora kwa yeye. 

Messi ambaye aliumia kwenye mechi waliyopata droo kwenye Laliga dhidi ya Atletico Madrid atakuwa nj'e kwa wiki tatu akiuguza majeraha yake.   

Fabregas alisema kuwa aliongea na nyota huyo wa Argentina na Barca baada ya kuwa nj'e.  

''Leo sijaongea na Messi, jana niliongea nae na nikamuuliza anaendeleaje na hakika yuko vizuri. Ni huruma ''alisema Fabregas.''  
''Atapona haraka.''  
 


No comments:

Post a Comment