Friday, September 23, 2016
ZIDANE KUCHAGUA KATI YA JAMES RODRIGUEZ, ISCO AU KOVACIC.
Kocha wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane itambidi afanye uamuzi wa kumchagua kiungo atakae ziba pengo la Casemiro ambaye atakuwa nj'e kwa wiki tatu baada ya kuumia mguu kwenye mechi dhidi ya Espanyol Jumapili iliyopita.
Na kutokana na hilo kumefanya Toni Kroos kuwa kiungo mkabaji wa nyuma na kuacha nafasi ya kiungo wazi ambayo mmoja kati ya hao watatu anaweza kuziba nafasi hiyo.
James Rodriguez ambaye alipata neema ya kuanza katika mechi dhidi ya Espanyol na Villarreal na kukabiliana vizuri na majukumu hayo aliyopewa, na kocha wake kupata amani.
Kovavic kwa upande mwingine, tayari ameshaziba nafasi ya Mcroatia mwenzake Luka Modric na kupata nafasi za kucheza, na ndie mchezaji pekee kati ya hao watatu anaeweza kucheza nafasi ya kiungo mkabaji. Huku wenzie wakiwa hodari zaidi kwenye kushambulia wakiwa na nia ya uchezeshaji zaidi ya kujua kukaba.
Wakati Rodriguez akiendelea kujiboresha, Isco yeye kupitia kuumia kwa Casemiro kunaweza kuwa bahati ya kuweza kupata nafasi ya kucheza.
Kuelekea mchezo dhidi ya Las Palmas, kuumia kwa Casemiro kumempa Zidane nafasi ya jinsi atakavyoweza kukipanga kikosi chake, na uchaguzi utakao hakikisha kuwa na maana kubwa kwa wachezaji ndani ya timu kwa siku zijazo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment