Saturday, September 10, 2016
GUARDIOLA AENDELEZA UBABE KWA MOURNIHO
Jose Mourniho amekubali kuendelea kuwa mnyonge kwa Pep Guardiola katika mechi wanazokutana baada ya leo kukubali kipigo cha magoli 2-1 nyumbani kwao Old Trafold. Lakini hilo halitamfanya Mreno huyo kukataa tamaa ya kufanya vizuri kwenye michezo yake inayofatia. Huku Guardiola akijiweka vizuri kwenye ligi hiyo kwa kutopoteza mechi toka ianze.
Ni Kevin De Bruyne alieanza kupeleka maumivu Old Traford,
Kevin De Bruyne akishangilia goli lake dhidi ya United.
Huku Kelechi Iheanacho akiitimisha maumivu zaidi kwa United kwa kuifungia City goli la pili.
Kelechi akishangilia goli lake.
Na Ibrahimovic alisawazisha lakini haikusaidia United kutoka kifua mbele nyumbani kwao.
City wanaongoza ligi hiyo kwa kufikisha pointi 12.
Na kwenye michezo mingine Liverpool imewafunga mabingwa wa msimu uliopita Leicester City 4-1 na Arsenal wakiokolewa na penati iliyowafanya watoke kifua mbele dhidi ya Southamption kwa goli 2-1, huku la Southamption likifungwa na kipa wa Arsenal Peter Cech aliejifunga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment