Monday, September 26, 2016

LIEWIG AACHANA NA STAND UNITED


Uongozi wa timu ya Stand United imevunja rasmi mkataba wake na kocha wao Patrick Liewig baada ya kuweza wazi kutoweza kulipa gharama za mshahara, malazi na mengineyo aliyokuwa akifanyiwa na klabu wakati ilipokuwa na udhamini wa kampuni ya uchimbaji madini ya AGACIA.
Liewig alikuwa na mkataba na Stand wa miaka miwili, na mpaka sasa ameshatumia mwaka mmoja akiwa kocha wa timu hiyo huku Agacia nayo ikivunja mkataba na Stand kutokana na migogoro ya viongozi kwenye timu hiyo, wakiwa wamebakiza mwaka mmoja wa mkataba wao kuisha kwa timu hiyo.    

Mfaransa huyo ambaye anatarajia kulipwa malipo yake yote ya uvunjwaji wa mkataba huo kwa maelezo ya mwanasheria wake Franck Nicolleau, huku timu ya Stand ikiandaa mkataba wa makubaliano ya kuvunja mkataba na Liewig unaoonyesha kuwa kocha huyo alisaini mkataba Julai 20, 2015. Na kupendekeza kumlipa mshahara wa mwezi mmoja jambo ambalo limekataliwa na mwanasheria wake. 

Mwanasheria huyo amedai kwamba Liewig anapaswa kulipwa pesa zake zote siku atakayo saini makubaliano ya kuvunja mkataba, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa na sheria za kazi zinaeleza kulipwa miezi 12 na si vinginevyo.  

Makubaliano ya kusaini mkataba huo yalipaswa yafanyike jana Jumapili baada ya mechi yao dhidi na Yanga. Huku Katibu Mkuu wa Stand Kennedy Nyagi akisema ''kweli mpango huo upo, tangu Agacia watangaze kujitoa mambo hayajakaa sawa na hatuwezi kumudu gharama, tulikubaliana mkataba tuuvunje na kocha alikubali.''   


  


No comments:

Post a Comment