Thursday, September 8, 2016

BRAZIL INAWEZA KUSHINDA ''WORLD CUP'' 2018 -COSTA


Mshambuliaji wa Brazil Douglas Costa anaamini taifa lake lina kiwango bora cha kushinda World Cup 2018 nchini Russia.
Taifa hilo la Amerika ya Kusini mara ya mwisho kushinda kombe hilo ilikuwa mwaka 2002, huku wakinyanyaswa kwenye ardhi ya nyumbani kwao miaka miwili iliyopita na Ujerumani baada ya kupokea kipigo cha aibu cha 7-1 kwenye nusu fainali.  

Lakini mwishowe walishinda medali ya dhahabu kwenye Olimpiki, ambayo imewatia nguvu Brazil na kuwapa heshima kama wenyeji wa michuano hiyo ambayo yamewafanya kukaa nafasi ya pili katika kufuzu CONMEBOL.    
 
  
Costa anajisikia kuwa chini ya kocha Tite, aliyechaguliwa June kukinoa kikosi hicho kuwa watakuwa na mafanikio mazuri nchini Russia. ''mimi ni bingwa wa dunia nikiwa na Brazil (2018).'' aliiambia Abendzeiting. Tuna kila kitu ambacho timu inahitaji. Kuna wachezaji wazuri na wakubwa kama Neymar na Philipe Countinho na kocha wetu mpya nae ni mzuri. Kama tukijikuta  kama timu basi tutakuwa miongoni mwa timu bora zaidi.  

Costa, ambaye alikosa michezo ya Rio sababu ya majeraha, ambayo pia yalimchelewesha pia kuanza kwenye msimu huu mpya na timu yake ya Bayern Munich. Nyota huyo wa zamani wa Shaktar Donetisk ambaye alihusishwa na mpango wa kuondoka kwa mabingwa wa Bundesliga mwanzoni mwa maka huu, alisema kuwa ana furaha kuwa Munich.   

''Hamna sababu inayonifanya niondoke Bayern, alisema Costa. Nina msimu mzuri, unaonifanya niendelee kutoa mchango wangu kwenye timu na kujisikia vizuri kuwepo hapa toka mwanzo.''    
 

Costa anatarajiwa kurudi kwa mara ya kwanza uwanjani toka aumie kwenye mechi ya Bayern dhidi  ya Schalke kwenye Bundesliga ijumaa hii.   




No comments:

Post a Comment