Thursday, September 8, 2016
UBORA WANGU NI KAMA WA MESSI NA RONALDO -SANCHEZ
Forward wa Arsenal Alexis Sanchez, anaamini kuwa yeye ni mchezaji bora kama wachezaji nyota wawili Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Sanchez ambaye alikuwa timu moja na Messi Barcelona, lakini aliondoka Nou Camp kuelekea ligi kuu ya England msimu wa 2014-2015 katika kutafuta nafasi ya kuanza kucheza baada ya kuonekana ugumu wa yeye kuanza Barca kikosi cha kwanza.
Nyota huyo wa Chile amekuwa mchezaji bora kwenye dimba la Emirates baada ya kufunga magoli 38 katika michezo 68 ya ligi aliyoonekana Gunners.
Messi na Ronaldo ni wapinzani ambao wanaonekana ni wachezaji bora kwenye ulimwengu huu wa soka kwa sasa, ambapo kwa kipindi cha miaka nane sasa wamekuwa wakipokezana tuzo ya mchezaji bora wa dunia ''Ballon d'Or'.
''Alisema kuwa nitafikia kiwango cha wachezaji hao,'' sijisikii kuwa duni kwa mtu yeyote na ninapenda kufananisha uwezo wangu kama wa Messi na Ronaldo. Nina uwezo sawa kama wao.
Sanchez ambaye alishinda La Liga na Copa del Rey akiwa na Barca, na huku pia FA CUP akiwa na Arsenal.
Vijana hao wa Arsene Wenger wanatarajia kushuka dimbani dhidi ya Southampton baada ya mapumziko ya mechi za Kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment