Wednesday, September 14, 2016

CEFERIN- USHINDANI ULIOPO BAINA YA CRISTIANO RONALDO NA LIONEL MESSI NI MZURI KWENYE SOKA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Ulaya (UEFA) Aleksandra Ceferin amesema kuwa ushindani uliopo baina ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi  kuwa ni mzuri kwenye soka.    

Rais huyo aliyasema hayo kwenye mahojiano yake na tovuti ya Marca ya nchini Spain alisema ''wote ni wachezaji wazuri kwenye soka,  kila mmoja ana vitu vizuri kumzidi mwenzake. Ronaldo ana nguvu na maamuzi na kwa Messi yeye ni zaidi ya msanii au fundi. Ni sawa na swali moja kati ya Real Madrid au Barcelona, wote ni wazuri kwa soka duniani.  

Pia walimuuliza kwanini aliamua kuwa Rais wa UEFA, nae alijibu kwamba ''nazani ninaweza kufanya mambo ya msingi kwenye soka. Siko hapa kwa ajili ya mapinduzi hata kidogo, lakini nadhani soka linahitaji mageuzi''. Wakati baadhi ya marais wa soka wa ndani wakiniambia kuwa UEFA inahitaji mabadiriko, nikafikria kuwa ni wakati wa kusaidia mpira wa miguu. Na ninaweza kufanya hivyo.  
  

 

No comments:

Post a Comment