Wednesday, September 14, 2016

ENYIMBA WAMSIMAMISHA KAZI OFISA WAO.



Mabingwa wa nchini Nigeria, Klabu ya Enyimba wametangaza kumsimamisha mmoja wa maofisa wake Ifeanyi Kalu kufuatia kutokea matukio kwenye Nigeria Professional Football League (NPFL) kwenye mechi yao dhidi ya Niger Tornadoes, Lokoja wikiendi iliyopita.  

Enyimba ambao walipoteza mchezo huo kwa 1-0 kwenye uwanja wa mashabiki uko Lokoja.   

Kalu amesimamishwa kutokana na klabu yake kueleza kuwa alifanya mambo yasiyokuwa ya kiungwana kama vile mtu asiefahamu soka. Pamoja na hilo pia amepigwa faini ya kukatwa mshahara wake wa mwezi huu kufuatia mambo aliyofanya, pia hatoruhusiwa kuwa kwenye benchi la kiufundi la klabu hiyo mpaka pale itakapotangazwa tena.     

''Enyimba Football Club binafsi inalaani vikali hatua na tabia yake kwa nguvu zote''.  Klabu yetu imejengwa katika nidhamu na heshima ya kuheshimu maofisa wa mechi na sheria za mchezo na hatuwezi kuvumiliana kwa chochote kitakachokuwa kinyume.''   

Mr Kalu aliomba radhi kwa yaliyotokea lakini hana budi kukubaliana na maamuzi ya klabu yake ya kukatwa mshahara wake kwa mwezi huu na kukaa mbali na benchi la ufundi la timu hiyo.  
 

 
      

No comments:

Post a Comment