Thursday, September 8, 2016

CONTE'S ''DAVID LUIZ KWANGU NI BEKI''


Masaa machache hapo jana baada ya nyota wa klabu ya Chelsea David Luiz kusema kuwa yuko tayari kucheza eneo lolote kwenye kikosi hicho, kocha wa klabu hiyo Antonio Conte, amesema kuwa hana mpango wa kumchezesha nyota huyo kama kiungo wa kati bali kwake ni beki.     

Luiz ambae amerudi Chelsea siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili akitokea Paris Saint-German ya Ufaransa, ambako alikuwa huko kwa misimu miwili na kushinda mara mbili ligi kuu ya Ufaransa ''Ligue 1''. Luiz ambae alisema kuwa ''niko hapa na kama atahitaji nicheze sehemu yoyote nitacheza''. 
 

Lakini Conte alisema najua kuna wakati anacheza kama kiungo wa kati na inakuwa vizuri kwa timu, lakini ningependa akilini mwangu, na mipango yangu kwake awe sehemu sahihi. Na kwangu atacheza nyuma kama beki. Kwa sasa tunahitaji kuimarisha safu ya ulinzi zaidi kwenye eneo la ulinzi.  
 

 

No comments:

Post a Comment