Monday, October 3, 2016

SONG APIGANIA MAISHA YAKE ICU

 


Nyota wa zamani wa Liverpool FC Rigobert Song mwenye umri wa miaka 40 anapigania maisha yake baada ya kukimbizwa hospitalini nchini Cameroon baada ya kupata shambulio kwenye ubongo na mpaka sasa yuko katika hali mbaya. 
Song ambaye ni mjomba wa mchezaji wa zamani wa Arsenal Alex Song alipatwa na shambulio la kiharusi ambalo linamfanya kupigania maisha yake ICU. Song alijiunga na Liverpool January 1999 kwa uhamisho wa euro milion 2.7 na kuichezea mechi 37 na kuondoka na kujiunga na West Ham 2000. 

Pia alizichezea klabu za Galatasaray, Koln, Lens, Metz na Trabzonsor, huku akishinda mechi 137 kwa Cameroon na medali ya dhahabu kwenye Olimpiki 2000. 

Song ni meneja wa timu ya taifa ya Chad.

Mchezaji mwenzake wa zamani wa liverpool Jamie Carragher na Robbie Fowler walionyesha majonzi yao kupitia akaunti zao za kijamii, 
  ''Natumaini kila kitu kitaenda sawa'' aliandika Carragher

 ''Mawazo yangu na familia ya Song. Natumaini atakaa sawa.'' aliandika Robbie Fowler.

No comments:

Post a Comment