Wednesday, September 14, 2016
EUROPA LEAGUE SIO NDOTO BALI TUNAHITAJI KUSHINDA -MOURINHO
Jose Mourinho ameonyesha nia yake ya kutaka kushinda Europa League akiwa na Manchester United na huku akijaribu kuangalia uwezekano wa kulichukulia umakini swala hilo licha ya kutokuwa na ushindani kwa wachezaji juu ya ndoto ya kutaka kucheza.
United ilishindwa kufuzu kwenye Champions League msimu uliopita baada ya kumaliza nafasi ya tano Premier League chini ya Louis Van Gaal.
''Ni mapema mno kuzungumzia kushinda mashindano haya, lakini sisi ni klabu kubwa na mechi ijayo ni muhimu kama unacheza Manchester United'', alisema Mourinho kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa kwanza dhidi ya Feyenoord Alhamisi hii.
''Europa League sio mashindano ya United kuwepo, sio ndoto ya kila mchezaji mkubwa. Lakini tunahitaji kushinda mashindano haya. Ni ngumu kufanya hilo lakini ni rahisi kusema hivyo na kujisikia kusema kwa sauti kubwa zaidi. Na hiyo ndiyo mbinu tunayotaka kutumia kwenye mashindano haya. Tumekuja kuheshimu wapinzani na upinzani, tumekuja japa kushinda mchezo.
''Nimekuja na kikosi kizuri na nitacheza na timu nzuri, baada ya kufungwa, jambo zuri ni kucheza na kila mtu anataka kucheza Alhamisi hii. Tunahitaji kuliangalia kwa heshima zaidi, nazani tunahitaji kufanya vizuri kwenye mashindano na matarajio ya klabu sio kuishia kwenye hatua ya makundi.''
United iko pamoja na timu za Zorya Luhansk na Fenerbance kwenye kundi A.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment