Thursday, September 15, 2016
SPORTING WANA NAFASI MOYONI MWANGU- RONALDO
Baada ya hapo jana kuwa mmoja wa wafungaji walioiwezesha Real Madrid kuanza vyema kampeni yao ya kutetea ubingwa wao wa Champions League kwenye ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Sporting CP, Cristiano Ronaldo ameelezea heshima aliyonayo kwa Sporting CP na kusema kuwa ndiyo maana hakuweza kushangilia goli lake aliloshinda jana dhidi yao.
Ronaldo aliewarudisha miamba hiyo ya Laliga kwenye mchezo kwa goli lake baada ya kuwa nyuma kwa goli 1-0 mbele ya wageni hao kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu kwa goli lake la dakika ya 89 kabla Arvalo Morata kufunga goli la ushindi ndani ya dakika za lala salama kwa timu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alishindwa kushangilia goli lake huku akielezea umuhimu wa Sporting CP juu ya kazi yake.
''Ilikuwa ni kupingana na timu ambayo nimejifunza biashara(kazi) yangu.''
''Hii klabu bado ina nafasi moyoni mwangu na ninaiheshimu sana.''
''Ndiyo maana sikuweza kushangilia dhidi yao.''
Bruno Cesar aliwaongoza wageni hao kuwa mbele kwa goli lake la dakika 47 kwenye mchezo huo Santiago Bernabeu lakini goli la Ronaldo na Morata aliyetokea benchi yaliwafanya vijana waZinedine Zidane kubaki na ushindi nyumbani kwao.
''Tulianza mechi taratibu , lakini kwenye mpira ndio ilivyo na ndio ilivyo kwa Real Madrid kurudi mchezoni ni sehemu katika uwanja huu,'' alisema Ronaldo.
Aliongeza kwa kusema kuwa ''mchezo huo umewapa onyo na hawatarudia tena kuanza mpira taratibu, sababu timu itapoteza muda na sisi na hatuitaji hilo.''
''Tunahitaji kumaliza kwa kuongoza kundi letu na kushinda.''
Real Madrid jumamosi hii wanakutana na Espanyol kwenye Laliga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment