Monday, September 26, 2016
FIFA SASA HIVI IKO IMARA ZAIDI- KATIBU MKUU FIFA FATMA SAMOURA
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani [FIFA] Fatma Samoura katika hotuba yake ya kwanza iliyokuwa kivutio katika Mkataba wa Soccerex jijini Manchester,
Fatuma aliahidi vikwazo zaidi juu ya ubaguzi wowote utakaofanyika katika michezo.
Mwanamke huyo wa kwanza kuwa Katibu Mkuu wa FIFA amebainisha kuwa wamejifunza kutokana na makosa yaliyopita.Na kusema kuwa FIFA kwasasa imekuwa bora zaidi kuliko mwaka mmoja uliopita.
Mwanamama huyo ambaye aliteuliwa mwezi May, anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika historia ya Shirikisho hilo toka miaka 112 iliyopita.
Na kama mkongwa wa mipango ya Umoja wa Mataifa [UN] alisema kuwa yeye alitumika katika migogoro nchini Siera-Leone na Kosovo.
Alisema ''ninaweza kutumia uzoefu wangu wa Umoja wa Mataifa wa kufanya kazi katika hali ya wengi wao wakiwa katika utata wa vita kwenye nchi katikati ya miaka ya 90.
''Katikati ya mitikisiko na mapambano ambayo watu walitulia kukiwa na mvua au mchezo wa soka.
''Mapumziko yao mengine yalikuwa kipindi cha Ramadhani na Christmas.''
Mwanamama huyo ambaye ni Msenegal alisema kwamba amejifunza mengi wakati wa miezi yake ya kwanza katika majukumu, na kufanya kazi kwa uwajibikaji na uwazi zaidi katika michezo.
Akizungumzia hali ya utata ya hivi karibuni juu ya uchunguzi wa rushwa alisema ''sisi ni shirikisho bora kuliko tulivyokuwa mwaka mmoja uliopita na tutaendelea kufanya maendeleo, tuko kwenye kulenga zaidi kipi bora juu ya Shirika na kuhakikisha fedha zinatumika ipasavyo.''
Kusukuma juu ya bidhaa ya FIFA imekuwa ''kuharibu na kubomoa'' huku akibaki na ukakamavu.
''Ndio bidhaa zetu zimepata shida juu ya uharibifu ulioonekana lakini uwepo wangu hapa unaonyesha kwamba FIFA ina nia ya kurejesha yote hayo.''
Aliendelea kusema kuwa uteuzi wake kama mwanamke wa kiafrika katika moja ya nafasi za juu za kusimamia ajira katika michezo ya kimataifa inaonyesha kuwa nyakati zinabadirika.
Lakini alisisitiza kuwa yeye sio mgeni na michezo.
''Kuwa mpya katika upande wa mambo ya utawala mimi ninajenga uhusiano lakini sio mgeni au mpya katika michezo.'' Uzoefu wake katika soka aliupata kutoka kwenye timu ya mumewe huko Senegal ambapo yeye alikuwa rais wa timu hiyo
Hotuba hiyo kuu ambayo ilikuwa ikifuatiliwa na Q&A na mwenyeji David Davies, pia iligusia juu ya kutokomeza ubaguzi na haja ya utofauti katika utawala.
Huku akiahidi kuzingatia juu ya nyasi za mizizi na mpira wa miguu kwa wanawake, na alisisitiza kuwa yeye aliweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya mtazamo wa FIFA.
Aliongeza kwa kusema kuwa ''nadhani mabaya yashapita na sisi kuweka uchunguzi nyuma yetu kwa sababu hatutaki kuwa na wasiwasi kwa kile kilichotokea katika siku za nyuma.
''Kitu muhimu ni kwamba sasa hatupaswi kurudia makosa.''
Naye mwenyekiti wa Soccerex Tony Martin, aliongeza kwa kusema ''Baada ya mtikisiko tumeshuhudia utafutaji wa utawala ambao Fatma amechukua juu ya wasifu mkubwa ambao kwa miaka mingi ulikuwa na changamoto kubwa.''
''Najua ulimwengu wa soka una furaha kusikia kile alichogundua toka achukue madaraka na mipango yake ni kujenga ubora na kuonekana zaidi kwa siku zijazo.''
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment