Monday, September 26, 2016

SIWEZI KUSHINDANA NA BENZEMA -GRIEZMANN


Kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amesema kwamba hawezi kushindana na Karim Benzema, na kutaka mshambuliaji huyo wa Real Madrid kupewa nafasi nyingine Les Bleus.
Benzema ambaye hakuwepo kwenye kikosi kilichocheza Euro 2016 kutokana na madai ya kuhusika kwake katika jaribio la usaliti kwa mchezaji mwenzake katika timu ya taifa Mathieu Valbuena.  

Griezmann ambaye ni kiungo wa Atletico Madrid amekuwa akisifiwa mwenendo wake nj'e na ndani ya uwanja. 

Griezmann ambaye alikiri kuwa hata yeye pia aliwahi kufanya makosa na kufungiwa kuichezea timu ya taifa ya vijana kwa muda wa miezi 13 baada ya kujihusisha na tukio lililotokea klabu ya usiku akiwa kambini na timu ya vijana ''Under-21'', kwa kwenda klabu huku akiwa na michezo miwili muhimu.  

Griezmann aliliambia jarida la  Parisien ''nini maana ya mimi kupambana na Benzema? wote tuna majukumu tofauti. 

''Tunahitaji kujua wakati ambao tunasahau. Kwamba kilichotokea wakati wa Ufaransa Under-21 kimenibadirisha. Nilikuwa nina miaka 18 au 19 kwa wakati ule, nilikuwa mtoto ambaye amefika kwenye ulimwengu wa mangwiji wa soka na kuzani ninaweza kufanya chochote ninachohitaji. 

''Lakini nimejifunza kutokana na makosa. Nimefanya kila kitu ili kubadirika, yote ndani na nj'e ya uwanja.

''Ni sawa kwa Patrice Evra .Watu huko nj'e walisema kwamba ana ushawishi mbaya kipindi nilichojiunga na timu ya taifa, lakini ukweli ni kwamba ni mtu mzuri na anaetuimiza kufanya vizuri wote kwenye timu.    

 ''Hatupaswi kusikiliza kila kitu kinachosemwa.'' 

Rais wa Shirikisho la Soka Ufaransa Noel Le Graet alisema uamuzi juu ya kumwita Benzema kwenye timu ya taifa mpaka pale atakapokaa na kocha mkuu wa ufaransa Didier Deschamps.


No comments:

Post a Comment