Monday, September 26, 2016

ZIDANE ACHOSHWA NA WAANDISHI WA HABARI.


Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kwamba yeye sio mjinga na Cristiano Ronaldo ni ana akili, wote wanahitaji kitu kimoja. 


Zidane ameyasema hayo baada ya kuona jinsi waandishi wa habari walivyo na maoni tofauti juu yao, lakini kocha huyo amewahikikishia kwamba wote wako kwa ajili ya kuangalia mafanikio. 

Hali hiyo ilitokea kwenye mechi dhidi ya Las Palmas ambapo Ronaldo alitolewa nj'e kwenye mchezo huo na kuonyesha hasira za wazi kwa kocha wake huyo, ambapo muda huo walikuwa wakiongoza lakini mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2.

''Kwa sasa hasira ni ya kawaida, wachezaji wote hawapendi kutolewa nj'e na nilifanya maamuzi kwa ajili ya manufaa ya mchezaji,'' alisema kocha huyo mbele ya waandishi wa habari.

''Tumeongea na wachezaji wote kikosini kuhusu hilo, na inatakiwa kuishi na hilo. Tuko hapa kwa ajili ya jambo moja. 

Madrid ambayo itakabiliana na Borrusia Dortmund kwenye Ligi ya Mabingwa, mechi ambayo inaonekana ni mtihani kwao katika hatua ya makundi. 

''Tunajua kabisa tunacheza dhidi ya timu gani, lakini sisi ni Real Madrid na milele tutajaribu kushinda kila mchezo.''

  



No comments:

Post a Comment