Bingwa wa ngumi aliyestaafu mwaka mmoja uliopita Floyd Mayweather amesema kuwa mpambano kati yake na McCregor hauwezi kutokea huku akielezea kuwa alimpa ofa nyota huyo wa UFC.
Hapo mwanzoni Mayweather aliweka uhakika wa kukutana uliongoni na nyota huyo wa UFC, lakini sasa amedai kuwa ameshindwa kukubaliana masharti na McGregor na amepoteza maslahi kwenye mpambano huo.
''Myweather alisema'' ni uchizi kwamba nazungumzia mpambano na McGregor wakati kuna wapiganaji kibao wanaotaka kupigana nae, lakini nilikuwa wa kwanza.''
''Nilijaribu kuweka mpambano kati yangu na McGregor,'' aliiambia Fight Hype.
''Hatuwezi kufanya hilo litokee kwahiyo inatubidi tuendelee na maisha yetu.''
Mayweather ambae alistaafu bila kupigwa mwaka mmoja uliopita kwa kushinda mapambano 49, lakini anatarajia kurudi ulingoni kwa ajili kwa pambano la 50.
Myweather mwenye umri wa miaka 39 anadai kuwa yeye ni nyota mkubwa kwenye ngumi na mchanganyiko wa karate.
Bondia huyo mstaafu alisema kuwa anajisikia heshima kuona jina lake likipewa ukubwa kwenye MMA ikiwa ajashindana na yeyote yule.
McGregor aligusia baada ya ushindi wake dhidi ya Nate Diaz mwezi uliopita kuwa mpambano wake utakaofatia hautakuwa wa UFC.
Huku akitarajiwa kurudi ulingoni pengine kwenye UFC 205 au UFC 207 jijini Las Vegas December 30 mwaka huu, kukiwa na uwezekano wa kupambana na Eddie Alvarez.
No comments:
Post a Comment