Tuesday, September 20, 2016
KILIMANJARO QUEENS KUWEKA HISTORIA LEO CECAFA?
Leo majira ya saa 3.30 mchana, Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara ''Kilimanjaro Queens'' inashuka dimbani kwenye fainali ya kwanza ya michuano ya Chalenji kwa wanawake CECAFA ambayo imefanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo jijini Jinja, Uganda.
Kilimanjaro Queens waliingia Fainali baada kuifunga 4-1 wenyeji Uganda kwenye nusu fainali iliyofanyika Jumapili, na watakutana na Kenya ambao waliwafunga Ethiopia 3-2. Huku wenyeji Uganda watacheza na Ethiopia kumsaka mshindi wa tatu.
Michezo yote inatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa FUFA Technical Center, Uganda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment