Sunday, September 25, 2016

GUARDIOLA AIPIGIA MAHESABU TOTTENHAM KWENYE MCHEZO WAO.

Kocha  wa Manchester City Pep Guardiola anaangalia mbele zaidi juu ya timu yake jinsi itakavyoivaa Tottenham kwenye mchezo wao ujao wa Premier League wakiwa wageni White Hart Park. 
 Vijana wa Guardiola wameendelea na muendelezo wao mzuri kwenye  mechi zao msimu huu baada ya hapo jana kuifunga  3-1 Swansea City. 

Mchezo wao White Lane Park Jumapili ijayo unatarajiwa kuwa mtihani kwao, huku Guardiola akiwa na msisimko juu ya mechi ya hiyo. 

''Kwenye kipindi cha pili, tulicheza vizuri sana,'' alisema Guardiola juu ya mchezo wao dhidi ya Swansea. 

''Kiukweli penati ilitusaidia sana kusonga mbele na baada ya hapo tukatawala na mchezo na kutengeneza nafasi nyingi. Tulistahili kushinda

''Nina furaha na ushind huu muhimu sababu sasa tuna michezo miwili kabla ya mapumziko ya mechi za Kimataifa. 

''Tuna mchezo wa Klabu ya Mabingwa dhidi ya Celtic  Jumatano ijayo na baada ya hapo tunaenda kukutana iliyokuwa timu nzuri bora kwa miaka miwiwli iliyopita White Lane Park.

''Tutaangalia jinsi kiwango chetu kitakavyokuwa pale.''  

Tottenham Hotspurs iko nafasi ya pili kwenye Ligi hiyo nyuma ya Man city. 




No comments:

Post a Comment