Sunday, September 25, 2016

RONALDO MECHI SITA BAO MOJA



 Ni kama vile nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameanza kwa kusuasua msimu huu baada ya kufunga bao moja tu katika mechi sita alizocheza.
Toka msimu wa 2009/2010, ambapo Cristiano Ronaldo alikuwa mchezaji mwenye thamani kubwa duniani baada ya kujiunga na Real Madrid, Mreno huyo alikuwa akianza msimu na mabao yasiyo na idadi mpaka sasa, lakini tofauti kwa msimu huu.

Kwa kipindi chake alichokuwa Santiago Bernabeu hajawai kuwa na mwanzo mgumu kwa Madrid hata kuwa na bao moja katika mechi sita alizocheza.

Alikuwa na rekodi na mbaya msimu wa 2010/2011 ambapo alianza na mabao matatu tu na alipata rekodi nzuri kwa kuanza na mabao kumi msimu wa 2014/2015.  

Huku akiwa ameshikilia tuzo ya mwanasoka bora wa dunia Ballon d'OR na tuzo ya mwanasoka bora wa ulaya aliyoipata baada ya kuisha kwa michuano ya Euro ambapo timu yake ya Ureno walikuwa mabingwa wa kombe hilo. 


No comments:

Post a Comment