Thursday, September 8, 2016

HALI TETE KWA REAL MADRID NA ATLETICO MADRID DHIDI YA RUFAA YAO FIFA



Shirikisho la Soka ulimwenguni (FIFA), limetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na vilabu vya Real Madrid na Atletico Madrid dhidi ya kuzuiliwa kufanya usajili kwa wachezaji kwenye dirisha la usajili. Kwa maana hiyo Los Blancos na Los Colchoneros hawawezi kusajili wachezaji katika madirisha mawili, mpaka adhabu yao itakapomalizika January 2018.   

Miamba hiyo miwili ilifungiwa na kamati ya nidhamu ya FIFA mwezu January kutofanya usajili kwa madirisha mawili kutokana na kukiuka kanuni za FIFA za usajil, kwa kufanya usajili wa wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18 ambao sio raia wa Hispania. Adhabu ambayo wataanza kuitmikia sasa ambapo awali walikataa rufaa, huku pia wakipigwa faini huku Real Madrid wakitakiwa kulipa pound 249,00 na Atletico Madrid pound 662,000 huku wakiruhusiwa kufanya usajili lakini hawaruhusiwi kuwatumia wachezaji hao hadi 2018. Ikumbukwe pia Barcelona waliwahi kukumbana na adhabu ya namna hii pia.        
 


 
 


No comments:

Post a Comment