Friday, September 9, 2016

KUELEKEA ''MANCHESTER DERBY'' TAMBO NA PRESHA ZATAWALA


Ikiwa kesho ni mechi ya mahasimu ''Mancester Derby'' kwenye ligi kuu ya England. Mechi hiyo ambayo inatarajiwa kutazamwa na mamilioni ya watu duniani, kutokana na makocha mashughuli wa timu hizo mbili na upinzani uliopo baina yao, Jose Mourinho ''Man U'' na Pep Guardiola ''Man City''. Ifahamike kuwa makocha hawa wote wawili walikuwa kwenye ligi kuu ya Hispania ijulikanayo kama La Liga, tena kwenye timu zilizokuwa na upinzani wa hali ya juu, Mourinho akiwa R. Madrid na Guardiola akiwa na Barcelona.   




Bila shaka uwepo wao kwenye ligi ya La Liga ulifanya kuboresha ligi hiyo ambayo kwa kipindi walichokuwepo kulifanya kuonekana ni Ligi bora. Na sasa wanakutana kwenye ligi kuu England tena kwenye timu ambazo ni mahasimu ambao wanatokea jiji moja la Manchester.  Na kufanya ligi hiyo kuanza kuonekana bora tena baada ya hapa katikati kupoteza umaarufu wake.    


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na presha kubwa kutoka kwa makocha, wachezaji na hata mashabiki wa timu hizi mbili. Kwani mchezo ambao umeteka hisia za watu wengi duniani, kwani tayari aliekuwa golikipa namba moja wa United Michael Schmeichel amewaelezea wapinzani wao hao, Man City kuwa kamwe hawawezi kuwa juu zaidi ya Man United na kuukosoa mfumo wa uchezaji wa Guardiola. 
 

''City haiwezi kuwa juu kama United, katika msimu wa hivi karibuni walikuwa juu lakini hilo kamwe haliwezi kuwafanya kuwa bora na juu ya Mashetani Wekundu  kama klabu kubwa zaidi duniani'' alisema Schmeichel. United walishinda FA CUP msimu uliopita, lakini wanapambana kuendeleza utawala wa Sir Alex Ferguson tangu kustaafu kwake mwishoni mwa msimu wa 2012-2013.    


Huku nyota wa Mashetani hao wekundu Ibrahimovic akituma video ya utani kwa golikipa wa City Claudio Bravo,kwenye akaunti yake ya instagram ikisema ''karibu Manchester, Hapa ni baadhi ya gia unazohitaji kujifunza, tutaonana jumamosi''. Hivyo utaona ni jinsi gani ambavyo mchezo huo ulivyo na presha kwa wachezaji wa pande zote mbili.   

                     akiwa na Mourniho, Real Madrid.



  
                                 akiwa na Guardiola, Bayern Munich.

Huku Xabi Alonso ambaye aliwahi kuwa chini ya makocha  wote hao wawili wakati akiwa na Mourniho (Real Madrid) na Guardiola (Bayern Munich), amesema kuwa makocha hao wameifanya mechi hiyo kuwa kubwa zaidi, huku kila mmoja akiwa na aina yake ya ufundishaji. Wote ni washindi wanao chukia kupoteza pia wanafanya kazi kwa bidii ndio maana wanafanikiwa.  
 

No comments:

Post a Comment