Tuesday, September 27, 2016

HATUOGOPI SAFARI YA MOSCOW-ALDWEIRELD


Nyota wa Tottenham Hotspurs Toby Aldweireld amesema kwamba hawana hofsu na hali ya vitisho juu ya mchezo wao wa leo Jumanne Septemba 27 kwenye Klabu ya Mabingwa dhidi ya CSKA Moscow.



Kikosi cha Mauricio Pochettino kimesafiri mpaka Urusi kwa ajili ya mchezo wao wa pili kwenye kundi G, wakiangalia uwezekano wa ushindi baada ya kupoteza kwenye mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa na Monaco kwenye mchezo wao wa kwanza.  

Majadiliano mengi kabla ya mechi hiyo ilikuwa ni ya wasiwasi wa usalama kwa mashabiki, na Spurs ikiwa timu ya kwanza kutokea England kuitembelea Russia toka yatokee mapigano baina ya mashabiki wa nchi hizo katika Euro 2016.   

Mashabiki wageni wakishauriwa kutovaa jezi za klabu yao nj'e ya uwanja wa CSKA Moscow, lengo likiwa kuwaepusha na mashabiki wakorofi.   

But Aldweireld ambaye alikutana na Spartak Moscow akiwa na Ajax kwenye kumi na sita bora za Europa Ligi msimu wa 2010/11, amesema kwamba wamejiandaa vyema juu ya mchezo huo. 

''Ni vigumu kuelezea lakini kwa Russia siku zote mambo huwa hivi, na haswa kwenye mechi za Klabu Bingwa,'' alisema.

''Na haswa ikiwa timu zingine za ulaya zikija, Uingereza pia. Tunahitaji kuangalia zaidi juu ya mchezo wetu uwanjani na hayo mengine hayapo katika mikono yetu. 

''Ni hali ambayo iko hapa. Lakini nikiringanisha sisi sasa hivi na Ajax, tulikuwa wadogo sana,  ambapo sasa tunajua kuwa kwenye Premier League jinsi ya kucheza mechi za ugenini. 

''Kwa hiyo hamna anaeogopa kucheza Moscow, na kucheza mchezo wetu ninajiamini.''    

CSKA alipata sare ya 2-2 na Bayern Leverkusen kwenye mechi yao ya kwanza katika kundi lao hilo.

No comments:

Post a Comment