Tuesday, September 27, 2016

PLUIJM AJIHAKIKISHIA USHINDI OKTOBA 1.

Image result for hans pluijm images



Licha ya kupokea kipigo cha 1-0 toka kwa Stand United, kocha wa Yanga Hans Pluijm amesema kwamba hana wasiwasi na kikosi chake kuelekea mchezo wake wa Oktoba 1  dhidi ya mahasimu wao Simba SC utakopigwa katika Uwanja wa Taifa. Dar es Salaam. 


Yanga ambayo imeenda kuweka kambi katika visiwa vya Pemba kujiandaa na mchezo huo ambao huwa wa kusisimua kila wanapokutana timu hizo.  

Pluijm alisema kwamba licha ya kupoteza mchezi wao dhidi ya Stand haimaniishi pia wataenda kupoteza mchezo wao unaokuja. Bali ni kama wamejeruhiwa na watamaliza hasira zao kwa Simba.  

''Mechi yetu dhidi ya Stand ni tofauti na Simba na kama kuna anayefikiria kwamba matokeo haya ya kupoteza kwetu yatakuwa na mchango wowote katika mchezo ujao atakuwa anajidanganya mwenyewe,'' alisema. 

Pluijm alisema anajua mbinu zote zitakazo muwezesha kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo, huku wachezaji wake wakiusubili kwa hamu mchezo huo.  

''Binafsi nadhani hata Simba wanaiogopa Yanga, hiyo itakuwa mechi tofauti kabisa nimewaona Simba ni timu iliyoanza kubadilika, lakini tunasubiri matokeo ya mwisho wa mchezo. 

Pluijm alisema kwamba wana timu imara na kilichotokea juzi ni sehemu ya matokeo ya soka walifanya kosa moja na wakapoteza , lakini walitengeneza walitengeneza nafasi nyingi. Na kwasasa hataki kusikia habari za viwanja kwani sio hoja mpya, na ana taarifa zote juu ya Simba ya sasa.

''Jambo lililonivutia ni kuwa wachezaji wangu wanajua umuhimu wa mchezo huo , hivyo tunachohitaji kukifanya ni kujua kucheza kwa akili na kuheshimu nidhamu ya mchezo tuna kikosi imara na halitakuwa jambo jipya tukishinda.'' alisema pluijm.    


No comments:

Post a Comment