Wednesday, September 7, 2016
INFANTINO ''HUENDA KOMBE LA DUNIA 2026 KWENDA AMERIKA YA KASKAZINI LIKIWA NA TIMU 40''
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (FIFA) Gianni Infantino ameweka bayana huenda Kombe la Dunia 2026 litafanyika Amerika ya Kaskazini. Mara ya mwisho mashindano hayo kufanyika barani humo ni mwaka 1994 nchini Marekani ambapo timu 24 zilishiriki.
Rais huyo wa FIFA amepanga kujadili juu ya uwepo wa timu 40 kwenye Kombe la Dunia kwenye mkutano wa Baraza la FIFA utakaofanyika tarehe 13-14 Oktoba jijini Zurich, wazo ambalo alikuwa nalo na kuliunga mkono toka kipindi chake cha kampeni kwenye kuwania cheo hicho kwenye Shirikisho hilo. Infantino ataongoza mkutano huo ambao ni wa kwanza kwa Baraza la FIFA na kujadili uwezekano wa kuongeza wajumbe 36 waliochaguliwa na mashirikisho sita.
''Niliwahi kusema kuwa, hakuna kikomo, kwa chochote kizuri kwa ajili ya Soka.'' alisema Infantino. Tutaangalia, lakini ni ukweli kwamba CONCACAF hawakuwa na Kombe la Dunia kwa muda mrefu.
''Kwa sasa nadhani kila kitu kiko wazi, maoni yangu juu ya timu 40 hayajabadirika.''
''Tumeona katika Euro nchini Ufaransa, timu nane zaidi, ni shauku ya aina gani hii inayotokana na nchi nyingi.'' Tunahitaji kutambua kwamba haya ni aina ya matukio zaidi kuliko ushindani, ni matukio ya jamii katika dunia nzima, aliongezea Infantino.
Kama Kombe la Dunia litapanuliwa na timu nyingi zaidi kushiriki basi litafuata nyayo za michuano ya Ulaya ambayo mashindano hayo yalikuwa na timu 24 kwa mara ya kwanza mwaka huu 2016 tofauti na ilivyozoeleka kuwa na timu 16 miaka iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment