Wednesday, September 7, 2016
RASHFORD APIGA ''HAT-TRICK ENGLAND U-21 IKIIUA NORWAY 6
Mchezaji kinda wa Man United Marcus Rashford amedhihirisha ubora wake kwa kocha wa timu ya wakubwa ya England Sam Allardyce ambae alimtema kwenye kikosi chake kilichocheza dhidi ya Slovakia jumapili iliyopita, baada ya hapo jana jumanne kufunga hat-trick kwenye ushindi wa mabao sita kwenye timu ya taifa ya chini ya umri wa miaka 21 dhidi ya Norway.
Rashford alikuwa mmoja kati ya wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha England kilichoshiriki michuano ya Euro 2016, lakini aliachwa na Allardyce kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Slovakia na kushinda bao 1-0 lililofungwa na Lallana kwenye mchezo uliokuwa mgumu kwao.
Kinda huyo ambaye ameshindwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Man u chini ya kocha Jose Mourniho, lakini kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi kuu msimu huu, akitokea benchi alifunga bao muhimu kwa mechi yake dakika za majeruhi dhidi ya Hull City na kufanya vijana wa Mourniho kushinda mechi zote tatu za kwanza za ligi hiyo England.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment