Wednesday, September 7, 2016
VIWANJA VITATU KUWAKA MOTO LEO VPL
Ligi Kuu ya Vodacom kuendelea leo kwenye viwanja tofauti na miji tofauti nchini. Ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea leo hii baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki kupisha mechi za mwisho za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Huku mabingwa wa ligi hiyo Yanga inatarajia kushuka dimbani kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara dhidi ya wenyeji wao Ndanda FC. Kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili kutokana na rekodi iliyopo baina yao, ambapo toka Ndanda ipande daraja na kushiriki ligi kuu haijawahi kufungwa na Yanga kwenye uwanja huo wa nyumbani kwao wa Nangwanda Sijaona. Kwani kila timu inataka kuweka rekodi,Yanga wanataka kuvunja mwiko kwa kuifunga Ndanda nyumbani kwao huku Ndanda wao wakitaka kutunza rekodi yao ya kutopoteza mchezo dhidi ya Yanga wakiwa nyumbani Nangwanda Sijaona.
Mchezo mwingine utakuwa kati ya Simba na Ruvu Shooting waliopanda daraja msimu huu, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru ''shamba la bibi'' mchezo ambao pia unatarajiwa kuwa na upinzani kutokana na timu zote mbili kuwa na pointi sawa kwenye msimamo wa ligi hiyo. Kwa mujibu wa Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kwamba mechi hiyo itakuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo leo hii.
''Napenda kuwafahamisha kuwa Uwanja wa Uhuru Dar es salaam umeanza kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza''amesema.
Huku washindi wa Ngao ya Jamii, Azam FC watakuwa wageni wa Prisons kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment