Wednesday, September 21, 2016

KIIZA AITWA THE CRANES KUZIKABILI TOGO NA GHANA.



Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Uganda Milutin Sredejovic ''Micho'' ameita wachezaji 30 katika kikosi kitakachozikabili Togo na Ghana mapema mwezi ujao.  

Huku akimjumuisha mshambuliaji wa Free States Stars Hamisi Kiiza kwenye kikosi hicho ambacho Oktoba 4 itacheza mechi ya kirafiki ya Kimataifa na Togo katika uwanja wa Kegue, Lome na itacheza na Ghana Oktoba 7  kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 katika kundi E.   

Hii ni mara kwanza kwa kocha huyo kukutana na waandishi wa habari toka wafuzu AFCON 2017. Micho aliwaambia waandishi hao kuwa sasa mtazamo wake mkuu ni kuwa makini  zaidi kwenye mechi zao hizo mbili muhimu kwa mwezi ujao.

''Shangwe baada ya kufuzu AFCON 2017 zinabaki kuwa zilizopita. Tutafanya kazi kwa ajili ya mikakati ya jinsi ya kuweza kufuzu, kwa sababu hii, mipango na maandalizi yanaanza mara moja. 

Kikosi cha Cranes kilichoitwa ni -

Goalkeepers: Dennis Onyango (Mamelodi Sundowns, South Africa), Salim Jamal (El Merriekh, Sudan), Benjamin Ochan (KCCA, Uganda), Ismail Watenga (Vipers, Uganda)

Defenders: Nicholas Wadada (Vipers, Uganda), Dennis Iguma (Al Ahed, Lebanon), Joseph Nsubuga (SC Villa, Uganda),  Isaac Isinde(St. George), Murushid Jjuuko (Simba, Tanzania), Rashid Toha (Onduparaka, Uganda), Timothy Awany (KCCA, Uganda), Halid Lwaliwa (Vipers, Uganda), Joseph Ochaya (KCCA, Uganda), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia, Kenya)

Midfielders: Mike Azira (Colorado Rapids, Uganda), Geofrey ‘Baba’ Kizito (Than Quảng Ninh, Vietnam), Aucho Khalid (Baroka, South Africa), Ivan Ntege (KCCA, Uganda), Moses Oloya (Kuban Krasnodar, Russia), Tonny Mawejje (Knattspyrnufélagið Þróttur, Iceland), William Luwagga Kizito (Rio Ave, Portugal), Abdulmalick Vitalis Tabu (SC Villa, Uganda)
 
Strikers: Hamis ‘Diego’ Kizza (Free State Stars, Uganda), Geoffrey Massa (Baroka, South Africa), Emmanuel Arnold Okwi (Sondjerskey, Denmark), Yunus Sentamu (Ilves, Finnland), Farouk Miya (Standard Liege, Denmark), Erisa Ssekisambu (Vipers, Uganda), Muhammed Shaban (Onduparaka, Uganda), Edrisa Lubega (Proline, Uganda.

 

No comments:

Post a Comment