Thursday, September 22, 2016

VILLARREAL WATIBUA REKODI YA REAL MADRID LA LIGA .

Karim Benzema na Cristiano Ronaldo wakiwa hawaamini kilichotokea Bernabeu
Hapo jana Real Madrid wamelazimishwa sare ya 1-1 na Villarreal na kutibuliwa rekodi yao ya kushinda mechi 17  mfululizo katika Laliga tena wakiwa kwenye uwanja wa kwao Estadio Santiago Bernabeu.   

Sergio Ramos aliokoa jahazi kwa goli lake la dakika ya 49 baada ya Villarreal kupata bao kupitia penati iliyopigwa na Bruno dakika ya 45. Matokeo hayo yanawafanya Madrid kubaki kwenye rekodi ya Pep Guadiola ya kushinda mechi 16 mfululizo katika Ligi akiwa Barcelona 2011. 

Huku wakiwa na nyota wao ambao hawakuwemo katika kikosi kilichocheza dhidi ya Espanyol, Ronaldo na Bale lakini hawakuweza kupenya ngome makini ya ulinzi yaVillarreal.

Pamoja na kukamilika kwa ''BBC'' lakini hawakuweza kuleta madhara kwa wageni hao mpaka pale Sergio Ramos alipowatoa kimasomaso na kuhaibika nyumbani dhidi ya wageni hao ambao walikuwa mbele kwa bao 1 walilolipata kipindi cha kwanza, iliwazimu Madrid kusubili mpaka kipindi cha pili kurudisha bao hilo. Na kufanya matokeo kuwa sare ya 1-1.

Madrid watashuka dimbani tena Jumamosi hii dhidi ya Las Palmas. 

No comments:

Post a Comment