Magoli ya kipindi cha pili ya Nikita Parris na Caren Carney dhidi ya Ubeligiji yaliweza kuwafanya timu ya Taifa ya Uingereza kumaliza hatua ya makundi wakiwa vinara katika kundi la saba bila ya kupoteza mchezo wowote na kufuzu Euro 2017.
Mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa timu zote, huku Ubeligiji ikipewa nafasi ya kuweza kuharibu rekodi ya Uingereza katika kundi hilo baada ya hapo mwanzo kutoka sare ya 1-1 Rothernham, mwezi April 2016. Lakini kipindi cha pili Uingereza walikitumia vizuri na kuweza kushinda wakiwa ugenini .
![]() |
Parris akishangilia bao lake dhidi ya Ubeligiji |
Parris aliitumia vizuri krosi ya Carney dakika ya 66 na kuifungia timu hiyo bao la kwanza na baadaye Carney aliifungia bao la pili.
![]() |
Carney akipongezana na mwenzie baada ya kufunga bao lake |
No comments:
Post a Comment