Tuesday, September 20, 2016

MICHO KUTANGAZA KIKOSI THE CRANES KITAKACHOZIVAA TOGO NA GHANA



Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uganda hapo kesho Septemba 21, litakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za shirikisho hilo FUFA,Mengo Uganda. 


Kupitia mkutano huo kocha wa timu ya Taifa ya Uganda ''The Cranes'' Milutin Sredojevic ''Micho'' anatarajiwa kutangaza kikosi kitakachosafiri kuelekea Togo na kitakachocheza na Ghana katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa FUFA, Ahmed Hussein alithibitisha mkutano huo.

''Kocha mkuu wa Uganda Cranes atakutana na waandishi wa habari Jumatano hii juu ya kutangaza kikosi kitakachocheza dhidi ya Togo na Ghana. Wakati huo huo mipango ya safari na maandalizi ya timu yatawekwa wazi. Wito kwa vyombo vya habari kuzingatia muda wa mkutano ambao utaanza saa 4 asubuhi.  

Uganda Cranes watacheza na Togo tarehe 4 Oktoba 2016 jijini Lome, kabla ya kukutana na Ghana tarehe 07 Oktoba 2016, jijini Tamale.  

No comments:

Post a Comment