Saturday, September 10, 2016
KILIMANJARO QUEENS YAENDA UGANDA KWA AJILI YA CECAFA
Baada ya hapo juzi Septemba 8, 2016 kuiburuza timu ya Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya Wanawake wa Tanzania Bara 'Kilimanjaro Queens', hapo jana ilitarajiwa kuondoka kuelekea Jinja, Uganda kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) maarufu kama Kombe la CECAFA ambayo itafanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016.
Burundi pia inakwenda Uganda ambako imepangwa makundi tofauti katika michuano hiyo. Tanzania kundi B ikiwa na timu za Rwanda na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na wenyeji Uganda.
Tanzania itafungua michezo hiyo kwa kucheza na Rwanda Septemba 12, 2016. Rwanda na Ethiopia zitacheza Septemba 14 2016, wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa kucheza na Burundi na siku hiyi hiyo, Uganda itacheza na Kenya.
Michezo mingine ya kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya zitakazo cheza Septemba 13 2016, ambako siku hiyo pia Zanzibar itacheza na Uganda. Septemba 15, 2016 Kenya itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa kucheza na Burundi.
Nusu fainali itafanyanyika Septemba 18, 2016, kabla ya fainali itakayo fanyika Septemba 20, 2016 itakayotanguliwa na kusaka mshindi wa tatu na nne.
Mashindano ya CECAFA kwa timu za wanawake yanafanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa Ukanda wa Afrika Mashriki na Kati. Tanzania ambayo ilianza kambi mwanzoni mwa Septemba kwa mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani kwa wiki moja na baadaye iliingia kambini rasmi kwa safari ya Uganda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment