Saturday, September 10, 2016

VPL KUENDELEA WIKIENDI HII


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwenye viwanja vitano tofauti kwenye michezo ya  mzungumko wa nne.  

Miongoni mwa mechi zitazoshuka dimbani ni pamoja na Ruvu Shooting watakao wakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi Mkoani Pwani, huku Mwadui FC ikimkaribisha Stand United kwenye uwanja wa Mwadui Complex Mkoani Shinyanga.    

Mabingwa wa ligi hiyo Yanga Afrika itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam. Huku Azam ikiendelea kuwa mgeni tena kwenye uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya dhidi ya Mbeya City, kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali baina ya timu hizo.Ndanda ikiwa nyumbani kwao kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona itacheza na Kagera Sugar ya Mkoani Kagera.  

Ligi hiyo itaendelea kesho Jumapili, September 11 2016 ambako kutakuwa na mchezo wa Simba itakayokuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro kwenye uwanja wa Uhuru. Huku mchezo wa African Lyon na Mbao umesogezwa mbele hadi Jumatatu Sep12 2016, kutokana na kubadilisha uwanja wa kuchezea ambapo hapo mwanzo ilibidi uchezwe kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na hivyo timu hizo zitakutana kwenye uwanja wa Uhuru.    

 

 

No comments:

Post a Comment