Monday, September 5, 2016

KOCHA MBEYA CITY AMFUNGULIA MILANGO NGASA


Kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri, anataka kuhakikisha anamsajili winga huyo katika kikosi chake. Kocha huyo ambaye ndie aliemsahinisha Ngasa Free States baada ya msimu wa 2014/2015 alisema kuwa yupo tayari kumpa mkataba hata leo kwani anamjua kuwa ni mchezaji mzuri. Ingawa Mmalawi huyo ameelezea hofu yake ya kumkosa kutokana na uwezo wake wa kumlipa mshahara mchezaji huyo.


''Hata kama ni leo hii akinihakikishia yupo tayari kujiunga na kucheza Mbeya City, nawaagiza viongozi kumpa mkataba, unajua mchezaji huru anaweza kujiunga na timu muda wowote hata kama usajili ukiwa umekwisha''.



''Ngasa ni mchezaji mzuri na aliyekamilika na ndio maana nilifanya juu chini asajiliwe Free States , japo sijajua nini kilitokea mpaka kufikia hatua ya kukatisha mkataba'' alisema kocha huyo.


Huku kukiwa na taarifa zikisema kuwa kamati ya Ufundi ya Yanga inakusudia kukaa kujadili kuona kama kuna uwezekano wa kumrejesha Mrisho Ngasa klabuni hapo. Japo kocha wa Yanga, Hans Pluijm kusema kuwa winga huyo hana nafasi katika kikosi chake lakini taarifa za ndani zinasema kuwa kamati imepanga kukutana na kujadili uwezekano wa kumrejesha kundini mchezaji huyo.
 
Ngasa aliondoka Yanga mwaka 2015 na kuelekea Free States ya Afrika Kusini, huvi karibuni alivunja mkataba na klabu hiyo na sasa yupo jijini Dar akiwa hana timu yoyote. Inasemekana Ngasa alilazimika kusitisha mkataba na klabu hiyo ya Afrika Kusini kwasababu ambazo hazijawekwa wazi. Ingawa taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Yanga, kuwa kabla ya mchezaji huyo kufikia hatua hiyo aliwaomba kutaka kumalizia soka lake Jangwani.




 

 

No comments:

Post a Comment