Monday, September 5, 2016

SIMBA YAREJEA DAR KUIVAA RUVU SHOOTING VPL




Kikosi cha Simba kimerejea jijini Dar es salaam hapo jana jumapili kikitokea mkoani Dodoma kilipokuwa kikijiweka fiti kwa ajili ya michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara. Nakusema kuwa wako fiti kwa mechi zijazo za ligi, na inatarajia kushuka dimbani jumatano hii dhidi ya Ruvu Shooting. Simba ilikuwa mkoani Dodoma baada ya kupata mualiko wa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Polisi Dodoma inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0. 



Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mganda, Jackson Mayanja, amesema kwamba safari hiyo ilikuwa muhimu kwao kipindi hiki ambacho ligi kuu ilikuwa imesimama, ni faida kwao kucheza mchezo huo kwani walijiweka sawa na kurekebisha makosa yao waliyoyaona hapo awali katika mechi zao mbili zilizopita, hivyo sasa hivi wako vizuri zaidi.


''Bado tuna safari ndefu na ligi ina mechi nyingi, kwa hiyo unapopata nafasi  kama hii na unapoitumia vizuri kurekebisha makosa yenu inaleta faida kubwa kwa mechi za baadaye, ukizingatia msimu huu tunahitaji kufanya vizuri zaidi'' alisema Mayanja.



''Mazoezi na mechi tuliyocheza, imekuwa na mchango mkubwa kwa maandalizi ya kujiweka fiti zaidi kwa ajili ya michezo ya ligi inayokuja, imekuwa vyema kupata nafasi ya kuja sehemu kama hii wakati ligi imesimama na kupata muda wa kurekebisha makosa tuliyoyaona kwenye mechi za awali za ligi''.


 Simba ambayo imecheza mechi mbili za ligi, ya kwanza ilikuwa dhidi ya Ndanda ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 3-0, na mechi ya pili wakatoka suluhu dhidi ya JKT Ruvu , kwa matokeo hayo wana pointi nne mkononi.



 
 

No comments:

Post a Comment