Tuesday, September 6, 2016
KUELEKEA KOMBE LA DUNIA, HISPANIA NA ITALY ZATAKATA
Hapo jana kulikuwa na michezo kadhaa ya kimataifa kuelekea kufudhu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018, ambapo timu ya taifa ya Hispania imeanza vyema harakati zake kwa kuifunga mabao 8-0 timu ya taifa ya Liechtenstein usiku wa kuamkia leo, huku nyota wa Chelsea Diego Costa akiwa kinara wa mabao hayo kwa kuifungia timu hiyo mabao 3, huku Alvaro Morata akifunga 2, na mabao mengine yalifungwa na Sergio Roberto 1, David Silva 1, na Vitolo 1.
Huku Italia ikiifunga Israel 3-1 kwenye mchezo ambao Italia walijikuta wakicheza pungufu baada ya beki wake Giorgio Chiellini kupewa kadi ya pili ya njano ndani ya dakika 55, ambaye atakosa mchezo utaofata dhidi ya Hispania tarehe 6 Oktoba.
Huku mechi ya Albania na Macedonia ikiahirishwa ndani ya dakika 77 ya mchezo kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na timu hizo mbili zilikuwa tayali zimeshafungana bao 1-1.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment