Tuesday, September 6, 2016

SERENA WILLIAM AVUNJA REKODI YA ROGER FEDERER US OPEN



Historia nyingine imeandikwa na mcheza tenisi namba moja kwa ubora duniani kwa upande wa wanawake Serena William, hapo jana baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Yaroslava Shvedova wa Kazakhstan kwenye mashindano ya US Open jijini New York nchini Marekani. Ushindi huo umemfanya kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mcheza tenisi kwa upande wa wanaume Roger Federer ya kuwa mchezaji wa muda wote alieshinda mara nyingi kwenye mchezo huo. 

 Ni siku nyingine na rekodi nyingine kwa Serena alievunja rekodi ya Federer ya kushinda michezo 307 dhidi ya kwake 308, na sasa anakuwa mchezaji wa muda wote alieshinda mechi nyingi kwenye mchezo huo wa tenisi.

''Ni idadi kubwa'', alisema William juu ya rekodi yake ya ushindi wa michezo 308 kwenye mchezo huo wa tenisi,''nadhani ni muhimu sana kwangu na sikufikiria kucheza mpaka sasa na sioni nitaacha lini''. 
Pia aliongeza kuwa anafurahia wakati huu kuweza kuvunja rekodi iliyokuwepo ambayo hakujua kama ilikuwa inawezekana kuvunjwa.


 






No comments:

Post a Comment