Wednesday, September 7, 2016
KUELEKEA KUFUZU KOMBE LA DUNIA UBELGIJI YANG'ARA,URENO YACHAPWA
Hapo jana kumekuwa na michezo iliyoendelea kwa ajili ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018, ambapo baadhi ya nchi zilishuka dimbani kuanza kampeni zao. Ambapo Ubelgiji ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wao Cyprus. Huku Romelu Lukaku akiibuka shujaa kwenye mchezo huo ambapo aliifungia timu yake mabao mawili kati ya matatu, na bao lingine lilifungwa naYannick Carrasco.
Huku Mabingwa wa Ulaya, Ureno wakipokea kipigo cha 2-0 kutoka kwa Uswisi kwenye mchezo uliopigwa St Jakob Park hapo jana. Mabao ya Uswisi yalifungwa na Embolo pamoja na mchezaji wa Bayern Leverkusen's Admir Mehmedi.
Huku vijana wa Didier Deschamps wameanza kwa matokeo mabaya kwa kusuasua kampeni hizo za kufuzu Kombe la Dunia, ambapo hapo jana walilazimishwa sare ya 0-0 na Belarus usiku wa jana.
Huku Wesley Sneijder akiokoa jahazi kwa timu yake ya Uholanzi kulala kwa Sweden ambao walitangulia kushinda na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Michezo mingine iliyokuwepo pia ni pamoja na Argentina bila nyota wao Lionel Messi,kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Venezuela huku magoli ya Venezuela yakiwekwa wavuni na Juan Anor na Josef Martinez, huku ya Argentina yalifungwa na Lucas Pratto na Nicolas Otamendi.
Huku Mabingwa wa Olimpiki 2016 Brazil wakiifunga Colombia 2-1, huku nyota wao Neymar akifunga kwenye mchezo huo na bao lingine likifungwa na Joao Miranda huku la Colombia likifungwa na Marquinhos. Na michezo mingine ilikuwa ni kama ifuatavyo, Uruguay 4- Paraguay 0, Chile 0- Bolivia 0, Peru 2- Ecuador 1.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






No comments:
Post a Comment