Wednesday, September 7, 2016

TIKETI ZA ELEKTRONIKI KARIBUNI KUANZA KUTUMIKA







Kwa mujibu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema tayari wameshakamilisha taratibu za mfumo wa utumiaji wa tiketi za elektroniki kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam na muda wowote zitaanza kutumika. Tiketi hizo zenye lengo la kuipatia Serikali mapato sahihi ya viingilio vya mechi kwenye viwanja vyake. 

Ni muda mrefu umepita toka serikali itangaze kuweka mfumo wa tiketi hizo kwenye viwanja inavyomiliki vya Uhuru ''shamba la bibi'' na Taifa, lakini suala hilo lilionekana kama kusuasua kabla ya hivi karibuni kulitilia mkazo na hatimaye kukamilika. 

Awali ilielezwa kuwa, jumapili iliyopita ndiyo serikali itakabidhiwa mfumo huo baada ya kukamilika, lakini zoezi hilo likaahirishwa kutokana na shughuli za kiserikali kuingiliana. 

''Kila kitu kimekamilika na nimehakikishiwa hilo na wale tuliowapa kazi hiyo, ile ratiba ya awali ya makabidhiano niliihairisha mimi na si mwingine kwa sababu siku tuliyopanga awali mimi nilikuwa Dodoma kwenye shughuli nyingine za kiserikali'' alisema Waziri Nape. Huku akisisitiza kuwa wikiendi hii ndiyo wanatarajia kufanya zoezi la makabidhiano.    
 

No comments:

Post a Comment