Friday, September 9, 2016

MASAU BWIRE AKEJELI KIWANGO CHA MAVUGO


Ofisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire, licha ya tambo zake na maneno yake kabla ya mchezo wao na wekundu wa msimbazi na kupokea kipigo cha mabao mawili baada ya mchezo wao na Simba, lakini bado ofisa habari huyo hajaacha machachari yake kwa wekundu hao wa msimbazi. Hapo awali kabla ya mchezo wao alijionyesha msisitizo wa kumuua mnyama ambapo alisema kuwa wanaenda kumfukuza simba kwa bakora sababu ana njaa hivyo hawezi kuwadhuru. 


Lakini walijikuta wakiraluliwa na mnyama kwa bao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru siku ya Jumatano ya wiki hii na kuwafanya maafande hao wa Ruvu kuondoka wakiwa mikono mitupu. Lakini hilo halikuweza kumfunga mdomo Bwire ambae kwenye mahojiano yake baada ya mechi kumalizika alieleza kuwa walicheza mpira mzuri lakini bahati haikuwa yao na kuponda kiwango cha nyota wa Simba Mavugo kuwa ni cha kawaida sana.

''Unajua kiwang cha Mavugo ni cha kawaida sana ila Watanzania wengi wanampaisha lakini ni mchezaji wa kawaida tena sana .'' Kiwango chake si cha kutisha na hata mabao yake anayofunga ni ya kawaida sana na hata lile alilowafunga ni la bahati, mabeki wetu  walijichanganya kidogo wakamuacha peke yake ndio akafunga. 

Ofisa habari huyo, alienda mbali zaidi kwa kusema ''mabao ya Mavugo yanaweza kufungwa na watoto wa darasa wa nne anaowafundisa soka, kwani rahisi mno sidhani kama kuna mtu anaweza kukosa akiwa eneo lile.''     

Mavugo ambae ameshafunga mabao mawili katika mechi zake tatu za ligi msimu huu, la kwanza likiwa dhidi ya Ndanda ambapo mnyama alishinda 3-1.  
 





      

No comments:

Post a Comment