![]() |
Simeone na Enrique wakisalimiana kwenye moja za mechi zao |
Kesho Septemba 21,2016 Ligi Kuu ya Hispania, Spain Primera Division maarufu kama La Liga inaendelea huku mechi ambayo inatarajiwa kutazamwa na wengi ni ya Atletico Madrid kwenda Barcelona Nou Camp. Timu hizo zitakutana na kuangalia jinsi ya kuifikia Real Madrid kwenye usukani wa ligi hiyo. Huku mara ya mwisho kukutana kwao ilikuwa kwenye Champions League ambapo Simeone aliibuka na ushindi wa 3-2.
Hii ni list za mechi baina ya makocha hao wawili walizowahi kukutana, huku Barcelona wakiwa na rekodi nzuri dhidi ya wapinzani wao hao.
Barcelona 3-1 Atletico (11/01/2015)
Kwa mara ya kwanza makocha hao kujaribu kuonyesha umwamba kwa mwenzake katika mechi hii ambayo Catalunya walitaka kulipiza kisasi kwa Colochonelos ambao waliwaacha bila Champions League au taji la ligi kwa misimu miwili iliyopita.
Na wakati huo kila memba wa MSN alifunga goli dhidi ya safu maarufu ya ulinzi ya Simeone.
Barcelona 1-0 Atletico (21/01/2015)

Bao la Lionel Messi liliwaokoa Barcelona kwenye nusu fainali ya Copa del Rey.
Atletico 2-3 Barcelona (28/01/2015)
Kwenye mechi hii Arda Turan akiwa Atletico alipoteza uungwana na kumrushia kiatu chake lainzmani, ingawa sasa hivi yuko kwenye kikosi cha Enrique na sio Simeone tena. Hii ilitokana na joto la upinzani baina ya mechi kati ya klabu hizo katika miaka ya hivi karibuni.
Atletico 0-1 Barcelona (17/05/2015)
Bao la Lionel Messi lilipeleka ushindi wa taji la Ligi kwa vijana wa Enrique kwenye uwanja wa Vicente Calderon.
Atletico 1-2 Barcelona (12/09/2015)

Messi na Neymar kama kawaida yao wakitoka nyuma ya goli la Fernando Torres na kuipa ushindi Barcelona.
Barcelona 2-1 Atletico (30/01/2016)
Kwenye mechi hii pia Blaugrana iliwabidi kutoka nyuma, na MSN ndio walifunga goli hizo kupitia Messi na Suarez.
Barcelona 2-1 Atletico (05/04/2016)

Barcelona walijitiahidi kumaliza mahesabu ya mchezo huu kwenye raundi ya kwanza, lakini Atletico nao walifanya mchezo huo kuwa mgumu kwa wenyeji hao kwenye Champions League.
Atletico 2-0 Barcelona (13/04/2016)
Kupitia magoli ya Griezman, Atletico walifanikiwa kuwatoa mabingwa hao kwenye hatua ya mtoano kwenye Champions League na kuingia nusu fainali.
No comments:
Post a Comment