Friday, September 9, 2016

KUMBE PSG ILITAKA KUMFANYA NEYMAR AWE GHALI ZAIDI


Baada ya Neymar kusaini mkataba wake mpya na Barcelona  harakati za Paris Saint-German kutaka kumsajili zilifika mwisho, lakini hapo mwanzo ilikuwa na lengo la kumsajili nyota huyo wa Barca kwani wakala wake alipokea ofa nzuri na ya ajabu kwa PSG juu ya Neymar kama tu angekubali kujiunga nao.     

Klabu hiyo ya Ufaransa kwa muda mrefu imekuwa ikimtaka mshambuliaji huyo hata kutoa ahadi ya mkataba wa mamilioni ya pound ili kumrubuni kuondoka Catalunya.   


Wakala wa mshambuliaji huyo Wagner Ribeiro amebainisha hayo kwenye mahojiano na ESPN Brasil jinsi ambavyo PSG walivyokuwa wakimtaka mtu wao.     


''Angeweza kuchuma Euro million 40 kwa mwaka baada ya makato ya kodi, lakini Neymar aliamua kuchagua kusaini upya Barca, licha ya kujua atavuna fedha kidogo''. PSG walikuwa tayari kumsajili kwa dau la Euro million 190. Man United walimtaka pia lakini PSG ndio waliokuwa na nia thabiti ya kumng'oa Nou Camp.  
 
Neymar ambaye alijiunga na Barca akitokea Santos mwaka 2013 kwenye uhamisho uliokuwa na utata, tayari ameshashinda taji la La Liga mara mbili, Copa del Rey mara mbili na Champions League 2015. Pia ni sehemu ya MSN inayoundwa na Lionel Messi na Luis Suarez.  
   
 Lakini chanzo cha habari cha PSG wamekanusha habari hiyo kwenye French daily kwa kusema huo wote ni uwongo mtupu. 


  
 


    
 

No comments:

Post a Comment