Friday, September 9, 2016

MFALME WA REAL MADRID AMERUDI


Huku klabu ya Real Madrid ikiwa na matumaini kuwa mchezaji wake nyota Cristiano Ronaldo atakuwepo kwenye kikosi kitakachocheza jumamosi hii dhidi ya Osasuna. Itakuwa habari njema kwa Real Madrid na kocha wao Zinedine Zidane, ambao walianza msimu. Na Jumamosi hii itakuwa inatimia miezi miwili toka siku aliyoumia akiwa kwenye fainali ya European Championship.    

Madrid ambao walionekana ilianza msimu kawaida kutokana na kukosekana kwa Mreno huyo. Na kukosekana kwake katika mechi za ufunguzi ni mara ya kwanza kwa Ronaldo tangu ajiunge nao mwaka 2009, ingawa Los Blancos wako kamili msimu huu, huku wakiyakosa magoli yake.    

Ronald ambaye ana magoli si chini ya 364 katika misimu saba iliyomruhusu kuvunja rekodi ya Raul ya mabao 323 ambayo alisubiri kuiweka kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.   

Akiwa na miaka 31, ameshachezea misimu nane kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu huku akiwa na shauku ya kutangazwa kama Mfalme wa  Real Madrid. Isipokuwa kwenye msimu wake wa kwanza alifunga magoli 33 kwenye mechi 35, ambapo baada ya hapo wakati wote amekuwa akifikisha magoli 50.  


Ikumbukwe kuwa kwenye msimu wa 2011-2012 alifikisha magoli 60 au zaidi.  
 Mafanikio haya yanatokana na changamoto kutoka kwa Luis Suarez na Lionel Messi, pamoja na wachezaji wenzake katika timu yao Karim Benzema na Gareth Bale, ambao wanamfanya kuwa na moyo wa kuendelea kuboresha maendeleo na mafanikio yake.   


 Msimu huu anatarajia kukutana na upinzani mkali kutoka kwa Welshman ambaye katika michuano ya hivi karibuni aliidhihirisha kuwa yeye ni streika bora kwa Real na nchi yake.    
Bale ambaye ameanza msimu mzuri katika suala la mabao , kutokana na mfumo wao wa BBC, hata hivyo alitamfanya Ronaldo kukata tamaa katika kudhihirisha kuwa yeye ni mfungaji bora kwa miaka saba iliyopita akiwa Real.  
  
Na tayari wachezaji wote wanaounda jina la BBC wamefanya mazoezi kwa ajili ya mechi yao ya kesho dhidi ya Osasuna.

 
Karimu Benzema, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wamejumuika na wenzao leo hii kwa ajili ya mchezo wa kesho. 
 
 

No comments:

Post a Comment